BIASHARA YA VIDOLE VYA MIGUU NCHINI ZIMBABWE: Ni nini hasa kinaendelea?
“Nchini Zimbabwe, watu wameanza kuuza vidole vya miguu yao kwa maelfu ya dola. Hii ni kutokana na gharama za juu za kimaisha na serikali kushindwa kutengeneza ajira.” Hii ni sehemu ya ujumbe ulioandikwa kwenye mtandao wa Twitter siku nne zilizopita kupitia akaunti ya @InnocentZikky, chapisho ambalo pia limeeleza kuwa vidole hivi huuzwa kwa dola kimarekani 20,000 kwa vidole vidogo (sawa na Milioni 46 ya kitanzania) na dola 40,000 kwa vidole gumba (sawa na Milioni 93 za kitanzania). Chapisho hili liliambatanisha maneno hayo pamoja na picha ya mguu usio na vidole vyote, picha mojawapo kati ya picha tatu. BBC imeripoti kuwa mwanablogu mmoja wa Zimbabwe amedai biashara hiyo inafanyika katika kituo kimoja cha maduka katika mji mkuu wa Harare. Tetesi zaidi zinasema kuwa vidole hivi hutumiwa na watabibu wa kitamaduni wakijulikana kama waganga bandia wanaohusishwa na imani za kishirikina. Waganga hawa hushutumiwa na waganga wa kienyeji wanaotambulika kwa jina la ‘sangoma’ katika baadhi ya ...