Posts

Showing posts from September, 2022

MALKIA ELIZABETH II

 Uingereza leo hii, baada ya zaidi ya miaka 70 imeshuhudia kuchomoza kwa jua pasi na Malkia Elizabeth II kuwa kwenye utawala. Mnamo Septemba 9 2022, Malkia Elizabeth II aliyedumu muda mrefu zaidi nchini humo alifariki akiwa Balmoral akiwa na umri wa miaka 96 baada ya kutawala kwa zaidi ya maiak 70. Hakuna kiongozi aliyewahi kuwa na uzoefu kama huu. Mamilioni ya watu duniani wameungana na Waingereza na watu wa mataifa mengine 14 aliyokuwa akitawala mpaka umauti ulipomfika katika kuomboleza kifo cha Malkia Elizabeth II. Malkia Elizabeth II ni nani has ana kwanini kifo chake kimewagusa wengi? Wasifu wa Malkia Elizabeth na historia ya maisha yake Elizabeth Alexandra Mary Windsor alizaliwa mnamo Aprili 21, 1926 katika jumba lililokuwa karibu na Berkeley Square jijini London. Alikuwa mtoto wa kwanza wa Albert, mwanamfalme Mtawala wa York na mkewe ambaye zamani alifahamika kama Lady Elizabeth Bowes-Lyon. Elizabeth na dada yake Margaret Rose (aliyezaliwa 1930) walilelewa katika mazingira ...