SENSA YA WATU NA MAKAZI 2022
Sensa ya watu na makazi ni nini? Kwa mujibu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Sensa ya watu na makazi ni utaratibu wa kukusanya, kuchambua, kutathmini na kuchapisha na kusambaza takwimu za kidemografia, kiuchumi na kijamii kuhusiana na watu wote na makazi yao katika nchi kwa kipindi maalumu. Ifikapo Agosti 23 mwaka huu, Sensa ya watu na makazi itafanyika nchini, ikiwa ni Sensa ya sita (Sensa zingine zilikuwa katika mwaka 1967, 1978, 1988, 2002, na 2012), Sensa ambazo hufanyika kila baada ya miaka kumi. Serikali imekuwa ikihamasisha na kuweka juhudi kubwa katika kuhakikisha watu wanajiandaa na wanajitokeza kwa wingi kuhesabiwa. Mnamo tarehe 08 mwezi Aprili mwaka huu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kupitia Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, alitoa agizo kwa viongozi kutoa elimu na mafunzo kwa wananchi ili wajitokeze na kushiriki katika Sensa ya Watu na Makazi wakati akizindua Nembo na tarehe ya Sensa ya mwaka 2022 katika Hoteli ya Go...