Posts

MALKIA ELIZABETH II

 Uingereza leo hii, baada ya zaidi ya miaka 70 imeshuhudia kuchomoza kwa jua pasi na Malkia Elizabeth II kuwa kwenye utawala. Mnamo Septemba 9 2022, Malkia Elizabeth II aliyedumu muda mrefu zaidi nchini humo alifariki akiwa Balmoral akiwa na umri wa miaka 96 baada ya kutawala kwa zaidi ya maiak 70. Hakuna kiongozi aliyewahi kuwa na uzoefu kama huu. Mamilioni ya watu duniani wameungana na Waingereza na watu wa mataifa mengine 14 aliyokuwa akitawala mpaka umauti ulipomfika katika kuomboleza kifo cha Malkia Elizabeth II. Malkia Elizabeth II ni nani has ana kwanini kifo chake kimewagusa wengi? Wasifu wa Malkia Elizabeth na historia ya maisha yake Elizabeth Alexandra Mary Windsor alizaliwa mnamo Aprili 21, 1926 katika jumba lililokuwa karibu na Berkeley Square jijini London. Alikuwa mtoto wa kwanza wa Albert, mwanamfalme Mtawala wa York na mkewe ambaye zamani alifahamika kama Lady Elizabeth Bowes-Lyon. Elizabeth na dada yake Margaret Rose (aliyezaliwa 1930) walilelewa katika mazingira ...

SENSA YA WATU NA MAKAZI 2022

  Sensa ya watu na makazi ni nini? Kwa mujibu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Sensa ya watu na makazi ni utaratibu wa kukusanya, kuchambua, kutathmini na kuchapisha na kusambaza takwimu za kidemografia, kiuchumi na kijamii kuhusiana na watu wote na makazi yao katika nchi kwa kipindi maalumu. Ifikapo Agosti 23 mwaka huu, Sensa ya watu na makazi itafanyika nchini, ikiwa ni Sensa ya sita (Sensa zingine zilikuwa katika mwaka 1967, 1978, 1988, 2002, na 2012), Sensa ambazo hufanyika kila baada ya miaka kumi. Serikali imekuwa ikihamasisha na kuweka juhudi kubwa katika kuhakikisha watu wanajiandaa na wanajitokeza kwa wingi kuhesabiwa. Mnamo tarehe 08 mwezi Aprili mwaka huu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kupitia Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, alitoa agizo kwa viongozi kutoa elimu na mafunzo kwa wananchi ili wajitokeze na kushiriki katika Sensa ya Watu na Makazi wakati akizindua Nembo na tarehe ya Sensa ya mwaka 2022 katika Hoteli ya Go...

BIASHARA YA VIDOLE VYA MIGUU NCHINI ZIMBABWE: Ni nini hasa kinaendelea?

 “Nchini Zimbabwe, watu wameanza kuuza vidole vya miguu yao kwa maelfu ya dola. Hii ni kutokana na gharama za juu za kimaisha na serikali kushindwa kutengeneza ajira.” Hii ni sehemu ya ujumbe ulioandikwa kwenye mtandao wa Twitter siku nne zilizopita kupitia akaunti ya @InnocentZikky, chapisho ambalo pia limeeleza kuwa vidole hivi huuzwa kwa dola kimarekani 20,000 kwa vidole vidogo (sawa na Milioni 46 ya kitanzania) na dola 40,000 kwa vidole gumba (sawa na Milioni 93 za kitanzania). Chapisho hili liliambatanisha maneno hayo pamoja na picha ya mguu usio na vidole vyote, picha mojawapo kati ya picha tatu. BBC imeripoti kuwa mwanablogu mmoja wa Zimbabwe amedai biashara hiyo inafanyika katika kituo kimoja cha maduka katika mji mkuu wa Harare. Tetesi zaidi zinasema kuwa vidole hivi hutumiwa na watabibu wa kitamaduni wakijulikana kama waganga bandia wanaohusishwa na imani za kishirikina. Waganga hawa hushutumiwa na waganga wa kienyeji wanaotambulika kwa jina la ‘sangoma’ katika baadhi ya ...

MIAKA MIWILI TANGU KIFO CHA GEORGE FLOYD: Namna kifo chake kilivyomfanya kuwa alama ya mapambano dhidi ya mauwaji na ubaguzi wa rangi.

Mei 25, 2020, miaka miwili iliyopita, majira ya saa mbili usiku George Perry Floyd Jnr, alinunua pakiti la sigara katika duka linaloitwa Cup Foods katika makutano ya mtaa wa 38 wa Mashariki na mtaa wa Chicago kule Minneapolis, Marekani. Mwajiriwa wa duka lile alimshutumu Floyd kuwa alinunua pakiti lile la sigara kwa noti feki ya $20 na kuamua kumripoti. Baada ya maafisa wa polisi kufika eneo la tukio, walimtia mbaroni Bw. Floyd na kuifunga mikono yake nyuma kwa pingu, kumsogeza kando ya gari lao walipomlaza chini kabla ya afisa mmoja kuamua kumkandamiza shingoni kwa kutumia goti lake mpaka mauti ilipomfika. George Floyd ni moja kati ya mamia, pengine maelfu ya watu waliouwawa kikatili kutokana na ubaguzi wa rangi (racism and white supremacy). Tofauti kubwa ni kwamba, muhanga wa safari hii katika mauwaji ya kikatili yanayosababishwa na dhana za kibaguzi, aliuwawa kikatili huku video iliyoonyesha mauwaji hayo kuanzia alipokamatwa mpaka kifo chake ikizua hisia za huzuni na mshtuko kwa w...

Ugonjwa wa 'Monkeypox': Je, tunapaswa kuwa na wasiwasi?

‘Monkeypox’ ni ugonjwa unaosababishwa na kirusi ambacho hutoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu (kitaalamu huitwa ‘viral zoonosis’). Huu ni ugonjwa wenye dalili zinazofanana na zile zilizokuwa zikionekana kwa wagonjwa wa ndui (smallpox), licha ya kuwa madhara yake mwilini sio makali kama yale ya ndui. Monkeypox kimsingi ni ugonjwa ambao umekuwepo katika Afrika ya Kati na Magharibi, sanasana katika maeneo ya misitu ya mvua ya kitropiki na umekuwa ukisambaa kuelekea maeneo ya mijini. Jamii kadhaa za wanyama zimetajwa kuathirika zaidi na kirusi cha ugonjwa huu wa ‘Monkeypox’ ikiwemo aina fulani ya nyani, jamii za chindi (squirrels), panya kutoka Gambia, na aina zingine kadhaa za wanyama. Kisa cha kwanza cha Monkeypox kiliripotiwa mwaka 1970 katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa mvulana wa miaka tisa katika kipindi ambacho harakati nyingi sana za kupambana na ugonjwa wa ndui zilikuwa zikiendelea huku visa zaidi vikiendelea kuripotiwa Afrika ya Kati Pamoja na Afrika Magharibi. Tang...

COVID-19: A Sanguine Prediction of the 'New Normal'

  “WHO has been assessing this outbreak around the clock and we are deeply concerned both by the alarming levels of spread and severity, and by the alarming levels of inaction.” These words were said by the WHO director-general, Dr. Tedros Adhanom Ghebreyesus at a media briefing on COVID-19 on March 11 th 2020. “We have therefore made the assessment that COVID-19 can be characterized as a pandemic.” he added. COVID-19 pandemic is an ongoing global pandemic of coronavirus disease 2019 caused by Severe Acute Respiratory Syndrome Coronavirus 2 (SARS-CoV-2). The novel virus was identified vfrom an outbreak in Wuhan, China, a city with over 11 million people in December 2019 as a strange new pneumonia. On January 30 th 2020, the outbreak of COVID-19 was declared a Public Health Emergency of International Concern (PHEIC) by the WHO. Globally, as of 5:22pm CEST, 25 th April 2022, there had been 507,501,771 confirmed cases of COVID-19, including 6,220,390 deaths reported to WHO [All acc...

MFUMUKO WA BEI YA MAFUTA: Namna vita ya Urusi na Ukraine inavyochangia kupanda kwa bei ya mafuta na hatua zinazochukuliwa na serikali kukabiliana na mfumuko huo nchini Tanzania.

Moja kati ya mijadala mizito iliyozuka mitandaoni katika siku za hivi karibuni ni suala la kupanda kwa bei ya mafuta hadi kufikiwa kiwango cha juu zaidi kuwahi kuwepo katika soko la dunia kwa takribani miaka 14 sasa. Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Mei 3 mwaka huu ilitangaza bei mpya kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli kutumika kuanzia Mei 4 hapa nchini. Huku hali ya taharuki ikizuka kutokana na bei hizo kuwa juu sana mfano, bei elekezi ya mafuta ya petroli kwa rejareja jijini Dar-es-salaam ikiwa ni Tsh.3,148/= na bei ya dizeli ikiwa ni Tsh.3,264/=, serikali imekwisha toa tamko bungeni juu ya hatua za dharura zitakazochukuliwa. Aidha, watu wengi wamekuwa wakihoji uwiano na uhusiano wa kupanda kwa bei ya mafuta na sababu kubwa inayoelezwa kuwa ndiyo chanzo; vita ya Urusi na Ukraine. Ni kwa vipi vita ya Urusi na Ukraine inapelekea mfumuko wa bei ya mafuta? Mnamo Februari 24 mwaka huu, nchi ya Urusi iliivamia na kuingia ndani ya mipaka ya nchi ya Ukraine kat...